Thursday 28 May 2015

Pombe yasababisha kifo cha Mteja,Mhudumu ahukumiwa kifungo…….



Muhudumu mmoja wa baa amepatikana na hatia ya mauaji, baada ya kumpa mteja wake jumla ya vipimo 56 vya pombe na kisha akafa. Raia huyo wa Ufaransa alimpa Renaud Prudhomme mwenye umri wa miaka 56, ''shoti'' 56 za mvinyo katika baa yake kwa nia ya kuvunja rekodi ya mywaji pombe nambari moja.
Marehemu Prudhomme aliyekuwa ameandamana na binti yake kujiburudisha, alipelekwa nyumbani akiwa mlevi chakari.
Inaarifiwa kuwa alikimbizwa hospitalini ambapo alipatikana ameaga dunia siku iliyofuatia.
Hata hivyo mahakama ilimpata na hatia mhudumu huyo Gilles Crepin, mwenye umri wa miaka 47, kwa kumchochea marehemu Prudhomme aendelee kubugia mvinyo ilihali alikuwa mlevi kupindukia.
Mahakama ilisema kuwa Crepin aliendelea kuandika nani anayeshikilia rekodi hiyo kwenye ubao uliotundikwa hadharani kwa wateja wake.
Sasa Crepin amehukumiwa kifungo cha nyumbani cha miezi minne,na kupigwa marufuku ya kufanya kazi katika baa yeyote kwa kipindi cha mwaka mmoja.

0 comments:

Post a Comment