This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Thursday 31 August 2017

WATU MAARUFU WADUKULIWA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM…..

Instagram imegundua dosari katika mfumo wake iliofichua nambari za simu za watu maarufu pamoja na anwani zao kwa wadukuzi wa mitandao.

CHUO CHATUMA DOLA MILIONI MOJA KWA MWANAFUNZI KIMAKOSA AFRIKA KUSINI….

Chuo Kikuu kimoja nchini Afrika Kusini kimesema kwamba kilituma kimakosa jumla ya randi milioni 14 ambazo ni sawa na dola milioni moja za Marekani katika akaunti ya benki ya mwanafunzi mmoja nchini humo.

WANAFUNZI KUFUNZWA KUHUSU NJIA ZA KUTOA TALAKA INDIA…

Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.

Tuesday 29 August 2017

VIDEO: KAMANDA MPYA DSM AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA...


Kamanda mpya wa kanda maalum ya Dar es salaam aliyeteuliwa hivi karibuni,mchana wa leo amezungumza na waandishi wa habari kujitambulisaha na kutoa namba yakeya simu.

MAMBO MAZITO USIYOYAJUA JUU YA MATETEMEKO YA ARDHI……

Hadi sasa haijagunduliwa teknolojia ya kuaminika, inayoweza kutabiri kutokea kwa matetemeko ya ardhi popote Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla. Akizungumza mwishoni mwa wiki ofisini kwake mjini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabriel Mbogoni alisema teknolojia hiyo haipo popote duniani.

WASIWASI AFRIKA KUSINI BAADA YA VISA VYA ULAJI WA NYAMA YA BINADAMU…..

Hofu imekumba kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini, baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.

LIVE: KESI YA UCHAGUZI KENYA..



Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni huko nchni kenya,inaendelea kusikiliwa katika mahakama nchini humo

VIDEO: LISSU, LHRC WAUNGANA KUPINGA KULIPULIWA OFISI YA MAWAKILI…………

Tundu Lissu na Kituo cha Haki za Binadamu zimeungana kwa pamoja katika kupinga kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za IMMMA Advocates.

WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI…..

Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.

MUUGUZI ADAIWA KUHUSIKA KATIKA VIFO VYA WATU 84 UJERUMANI………….

Muuguzi mmoja anayetumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwauwa wagonjwa wawili kaskazini mwa Ujerumani, sasa anashukiwa kuhusika na visa 84 vya mauaji.

HUYU NI MTU ANAYEFUNZA KOMPYUTA KUTAMBUA HARUFU…

Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.

Monday 28 August 2017

VIDEO:POLISI WAZUNGUMZA KUHUSU KULIPULIWA OFISI ZA MAWAKILI…

Kufutaia tukio la kulipuliwa kwa ofisi za immma advocates, ambazo inaelezwa kuwa hutumiwa pia na wakili fatma karume.

MHASIRIWA WA UBAKAJI INDIA, MWENYE UMRI WA MIAKA 13 AIOMBA MAHAKAMA KUAVYA MIMBA….

Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 mhasiriwa wa matendo ya ubakaji kutoka mji wa Mumbai huko India, wamekwenda katika mahakama kuu ya nchi hiyo, kuomba idhini ya kuavya mimba aliyo nayo binti wao.

UPINZANI WARUHUSIWA KUKAGUA MITAMBO YA TUME YA UCHAGUZI KENYA………..

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeukubalia muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.

HOMA YA NGURUWE TISHIO NCHINI INDIA…


Mlipuko wa Homa ya Nguruwe ulioikumba India umesababisha vifo vya watu 1,094, kwa kipindi cha miezi minane iliyopita huku ikisemekana kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi na unasambaa kwa kasi.

Friday 25 August 2017

MKUU WA SAMSUNG AFUNGWA JELA MIAKA 5….

Mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni Samsung Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa.

MFUNGWA AUAWA KWA KUTUMIA SUMU MPYA FLORIDA, MAREKANI…..

Mzungu mtetea ubabe wa wazungu ambaye akliwaua watu kwa sababu ya asili yao miaka 30 iliyopita ameuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu.

MADAKTARI MBARONI KWA KUUZA VIUNGO VYA BINADAMU…..

Serikali ya Misri imewakamata madaktari ambao wanatuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara ya kuuza viungo vya binadamu.

WENYE VVU WAKITUMIA VIZURI ARVS HAWAWEZI KUAMBUKIZA...

Wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kufubaza virusi (ARVs), wamethibitika kitaalamu kuwa wakitumia dawa hizo kwa uaminifu bila kukatisha dozi, hawawezi kuwaambukiza watu wengine kwa kujamiiana.

Thursday 24 August 2017

VIDEO: KITUO CHA SHERIA CHATOA TAMKO LA KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI….

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, leo kimekutana na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,na kutoa Tamko kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini yanayosababisha uvunjifu wa haki za binadamu.

MWANAFUNZI AFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI NA DALADALA MOROGORO…

Mtu mmoja amefariki na wawili wamejeruhiwa baada ya gari ya abiria kugonga treni eneo la Tanesco Morogoro.

RAIS AIDHINISHA HIFADHI KUBWA ITUMIWE KWA UCHIMBAJI MADINI…

Serikali ya Brazil imefutilia mbali hifadhi kubwa ya taifa katika eneo la Amazon ili kutoa fursa ya uchumbaji wa madini katika eneo hilo.

SAMSUNG WAZINDUA TOLEO JIPYA LA GALAXY…

Kampuni ya simu za mkononi ya Sumsung, imezindua simu yake mpya ya Galaxy Note 8, ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye ushindaji zaidi katika soko.

Tuesday 22 August 2017

INDIA YAPIGA MARUFUKU TALAKA YA KUTAMKA TU…

Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake.

WASHTAKIWA KWA KULA NYAMA YA BINADAMU…..

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

Saturday 19 August 2017

NEW VIDEO:ROMA & STAMINA-HIVI AMA VILE

Roma na Stamina kupitia umoja wao ‘Rostam’ ameachia video ya ngoma yao mpya ‘Hivi Ama Vile’, video imeongozwa na Nicklass, audio ni Mr. T Touch.

MWANAMKE MTANZANIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA INDIA….

Mamlaka katika Mji wa New Delhi, India zimearifu kuwa zimewakamata Wanawake wawili wa Kiafrika baada ya kuwakuta na Dawa za Kulevya aina ya cocaine yenye thamani ya Dollar Milioni 6 za Marekani.

POLISI WAANZISHA MSAKO MKALI KUWATAFUTA WALIOMUUA WAYNE LOTTER……….

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linaendelea na msako mkali kuwatafuta watu waliompiga risasi na kumuua Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation, Wayne Lotter jijini Dar es Salaam juzi.

ZAIDI YA WATOTO 35,000 WAPATA CHANJO YA POLIO SYRIA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO kwa kushirikiana na wadau wengine wamekamilisha duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa polio nchini Syria.

SERIKALI YAKIRI KUNA MGOGORO WA BOMBADIER....

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa majibu kuhusu taarifa za mgogoro wa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu inayonunuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka kampuni ya Bombadier ya Nchini Canada.

LAGOS NI MJI WA PILI MBAYA ZAIDI KUISHI DUNIANI...

Mji wa Lagos nchini Nigeria umeorodhwa wa pili mbaya zaidi kuishi duniani na jarida la The Economist.

VIDEO: LISSU APASUA JIPU JUU YA BOMBARDIER ......

Lissu aizulia jambo Bombardier, mwanasheria huyo wa Chadema amedai ndege hiyo iliyonunuliwa na Serikali imezuiwa Canada.

UMMY MWALIMU AAGIZA KUBORESHWA KWA HUDUMA ZA AFYA…………

Serikali imewataka watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai kilichopo Wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.

UTAFITI: WATOTO WA KWANZA KUZALIWA HUWA NA AKILI ZAIDI KULIKO WADOGO ZAO……

Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa watoto wa kwanza kuzaliwa katika familia huwa na akili sana ukilinganisha na watoto wanaofuatia kuzaliwa.

FARU ALIYESOMBWA NA MAFURIKO KUTOKA NCHINI NEPAL HADI INDIA AOKOLEWA

Faru kutoka familia ya wale walio kwenye hatari ya kuangamia ambaye alisombwa na mafuriko kutoka nchini Nepal hadi India ameokolewa na kurudishwa nyumbani.

Thursday 17 August 2017

PETE ILIOPOTEA KWA MIAKA 13 YAPATIKANA KATIKA KAROTI….

Mwanamke mmoja wa Canada alipata karoti ya ziada na pete ya almasi baada ya kupatikana katika shamba lake la mboga miaka 13 baada ya kuipoteza.

Wednesday 16 August 2017

MABILIONI YA ESCROW YALIYOTOROSHWA KUREJESHWA NCHINI….

Timu kabambe ya uchunguzi ikiongozwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itahakikisha kila senti iliyofichwa nje ya nchi inarejeshwa ili haki iweze kutendeka kwa wahusika.

ZIMBABWE:NI LAZIMA KILA MTU APIMWE UKIMWI….

Rais wa Zambia Edga Lungu amesema kuwa kwa sasa ni lazima kila mtu apimwe hali yake ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.

MKAPA MIONGONI MWA WAATHIRIWA WA UPANUZI WA BARABARA...

Nyumba inayoaminika kumilikiwa na mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Benjamini Mkapa itavunjwa ili kuruhusu upanuzi wa barabara ya Morogoro.

UBAKAJI WAITAFUNA UNGUJA..

Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, inakabiliwa na kasi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi, ikiwemo matukio ya ubakaji na mimba kwa wanafunzi.

Friday 11 August 2017

KIPINDUPINDU CHAANZA KUSAMBAA MBEYA..........

Wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiendelea kuwatesa wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani hapa, ugonjwa huo umepiga hodi ndani ya jiji la Mbeya na hadi leo Alhamisi wagonjwa watano waligundulika.

VIDEO MPYA:ROMA ASIMULIA ALIVYOTEKWA….

Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.

Thursday 10 August 2017

FACEBOOK KUJA NA RUNINGA YA MTANDAONI..

Kampuni kubwa zaidi ya mitandao ya kijamii duniani Facebook, inatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”watch” ama tazama.

UNAWEZA KUSAFIRI UKITUMIA NDEGE ISIYO NA RUBANI....?

Hilo ndilo swali mamilioni ya watu huenda wakajiuliza siku za usoni ikiwa wanataka kusafiri kwenda likizo kote duniani.

Thursday 3 August 2017

UTAFITI: RAILA APATA USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA UHURU...

Wakati matokeo ya tafiti mbalimbali yanaendelea kutolewa kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya, matokeo ya utafiti mpya uliofanywa na Infotrak, unaonesha mgombea wa kambi ya upinzani ya NASA Raila Odinga angepata ushindi mwembamba dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kama uchaguzi ungefanyika jana.

UTAFITI: IDADI YA WATU WALIO NA UPOFU KUONGEZEKA DUNIANI...

Ripoti mpya imesema idadi ya watu wanaopata upofu duniani kote inaweza kuongezeka mara tatu.
Utafiti uliochapishwa kwenye Lancet ambalo ni jarida la afya linaloangalia afya ya dunia linatabiri

Wednesday 2 August 2017

KAMPUNI YA CHINA YASHTAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA GAMBIA…..

Wanamazingira kutoka miji midogo ya pwani nchini Gambia wameipeleka kampuni moja ya China mahakamani kwa madai ya kutupa takataka za sumu kwenye bahari.

BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUMEWE BAADA YA NDOA

Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani, ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.

MKUU MPYA WA FBI APATIKANA……

Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI.

Tuesday 1 August 2017

RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31

Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafanya kupata matibabu nchini Uingereza mwaka huu.