Tuesday, 29 August 2017

WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI…..

Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika, ambapo amesema kuwa waalimu wa wanafunzi hao wamekiuka maadili ya ualimu, na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia kama hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.

Amewataka wazazi kuwafatilia watoto wao kwa kila hatua, wajue wanafanya nini shuleni na kama mzazi hamfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita.


Hata hivyo kwa upande wa Afisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato, amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment