Saturday 19 August 2017

UMMY MWALIMU AAGIZA KUBORESHWA KWA HUDUMA ZA AFYA…………

Serikali imewataka watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai kilichopo Wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani hapo ya kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili
Amesema kuwa wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba, wigi wa proteini pamoja na vihatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha uzazi pingamizi hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua
 “Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”


Hata hivyo, Kwa upande wa madawa Ummy amesema kuwaa hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF

0 comments:

Post a Comment