Thursday, 3 August 2017

UTAFITI: IDADI YA WATU WALIO NA UPOFU KUONGEZEKA DUNIANI...

Ripoti mpya imesema idadi ya watu wanaopata upofu duniani kote inaweza kuongezeka mara tatu.
Utafiti uliochapishwa kwenye Lancet ambalo ni jarida la afya linaloangalia afya ya dunia linatabiri
watu watakaopata upofu wataongezeka kutoka milioni 36 waliopo sasa na kufikia watu milioni 115 ifikapo mwaka 2050 kama matibabu hayataboreshwa.
Watafiti wanasema idadi ya watu duniani wanaokabiliwa na tatizo la kutokoona limepungua katika miaka ya hivi karibuni, lakini idadi hiyo inaweza kubadilika kwa jinsi watu watakavyokuwa wanaishi miaka mingi na idadi ya watu duniani itakapoongezeka.
Maeneo yanayotajwa kuwa na matatizo makubwa ni Kusini na Mashiriki mwa bara la Asia, huku nchi za eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika nazo zikiwa na idadi kubwa pia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment