Wednesday 2 August 2017

MKUU MPYA WA FBI APATIKANA……

Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI.

Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Donald Trump mwezi May kufuatia uchunguzi aliokuwa akiufanya kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi Rais Trump.
Christopher Wray ni mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa mahakama ya nchi hiyo ambaye alifanya kazi chini ya Rais George Bush.
Bwana Wray amepata uungwaji mkono kutoka vyama vyote kwenye Kamati ya Sheria ya Bunge la Seneti wakati wa kikao cha kuthibitishwa kilichoketi mwezi uliopita ambapo alionyesha kuitii Katiba

0 comments:

Post a Comment