Friday, 11 August 2017

VIDEO MPYA:ROMA ASIMULIA ALIVYOTEKWA….

Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.

Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake,  watu anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la upelelezi wa tukio hilo.
Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.
Pia, rapa huyo  amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa amemtukana mkuu wa nchi.
Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane kwa hoja.
‘Zimbabwe’ imerekodiwa ndani ya Tongwe Records chini ya upishi wa Bin Laden.
Video inayoonesha muziki umehamishiwa maeneo ya malishoni imeongozwa na Nicklass,itizame hapo chini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment