Tuesday 1 August 2017

AMUUA MUMEWE KISA AMEWAHI KUINGIA BAFUNI...

Mgini Aron 37 mkazi wa Magunga Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mkewe Jeni Mwenda 25, kwa sababu ya wivu wa mapenzi.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Jafari Mohamed, amesema tukio hilo lilitokea Julai 30 majira ya saa 11:15 jioni katika kitongoji cha Kitaramanka Kata ya Mirwa.
Amesema baada ya marehemu kutoka matembezini alifika nyumbani moja kwa moja na kuingia bafuni, kitendo kilichomkasirisha mkewe akidai kwanini amerudi na kuingia bafuni moja kwa moja.
Kamanda Mohamed amesema baada ya marehemu kuambiwa hivyo walianza ugomvi na mpenzi wake huyo, katika purukushani ndipo Jeni alipomchoma na kitu chenye ncha kali upande wa titi la kushoto na kusababisha kifo chake.
Kamanda amesema mtuhumiwa ameshakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa uchunguzi zaidi.

0 comments:

Post a Comment