Timu kabambe ya uchunguzi ikiongozwa na wataalamu kutoka Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itahakikisha kila
senti iliyofichwa nje ya nchi inarejeshwa ili haki iweze kutendeka kwa wahusika.
Msako huo wa nchi za nje
unatokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wanufaika wa mgawo wa mabilioni
hayo kuwa walitoroshea fedha hizo barani ulaya na maeneo mengine mbalimbali
duniani.
Aidha, harakati hizo za
uchunguzi zinalengo moja tu kwamba hakuna fedha inayohusishwa na tuhuma hiyo
ambayo haitafikiwa ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zikizungumziwa bungeni
zilizochotwa kwenye benki kwa mifuko ya sandarusi na ile ya rambo.
Imeelezwa kuwa eneo kubwa
ambalo limelengwa na uchunguzi huo ni bara la Ulaya ambako inasemekana ndio
kuna kiasi kikubwa cha fedha kimehifadhiwa na wanufaika wa mgawo huo.
“Ni kweli tuna maofisa
wetu wa takukuru wamekwenda nje ya nchi kufuatilia fedha za Escrow, kwa sasa
siwezi kutaja kuwa ni nchi gani hasa tunazozifuatilia maana huu ni
uchunguzi,”amesema Mussa Misalaba Ofisa Mahusiano wa Takukuru.
0 comments:
Post a Comment