Wednesday, 2 August 2017

BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUMEWE BAADA YA NDOA

Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani, ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.

Kate Elizabeth Prichard mwenye umri wamiaka 25, alikuwa bado amevalia gauni la harusi wakati alipokamatwa katika hoteli moja katika mji wa Murfreesboro.
Alidaiwa kuchukua bunduki aina ya pistol na kuiweka kwenye kichwa cha mumewe na kufyatua.
Bunduki haikuwa na risasi lakini baadae alidaiwa kuijaza risasi na kufyatua angani, jambo lililowafanya waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kukimbia.
Walioshuhudia tukio hilo walitoa taarifa kwa polisi ndipo polisi walipowasili eneo la tukio.
Walisema wawili hao walikuwa wakinywa pombe nje ya hoteli.
Sajenti polisi katika mji wa Murfreesboro Kyle Evans amesema kuwa maharusi hao wote wawili hawakutoa ushirikiano kwa mamlaka husika juu ya tukio nhilo.

Sajenti Evans amesema kuwa bibi harusi alijaribu kuficha silaha bafuni katika hoteli walimokuwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment