Monday, 28 August 2017

HOMA YA NGURUWE TISHIO NCHINI INDIA…


Mlipuko wa Homa ya Nguruwe ulioikumba India umesababisha vifo vya watu 1,094, kwa kipindi cha miezi minane iliyopita huku ikisemekana kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi na unasambaa kwa kasi.



Idadi ya watu waliofariki kwa mwaka huu ni mara nne zaidi ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016, ambapo maambukizi ya ugonjwa huo yalikuwa yameshuka sana.

Aidha katika Jimbo la Maharashtra lililopo magharibi mwa nchi hiyo, ndilo lililoathirika zaidi ambapo waliofarikini kutokana na ugonjwa huo ni takribani watu 437 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya nchini humo.

Hata hivyo Mlipuko mbaya zaidi wa homa hiyo ambao uliikumba nchi hiyo ulitokea miaka ya 2009-2010, ambapo watu 50,000 waliambukizwa na wengine 2,700 kufariki dunia nchini humo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Matibabu katika hospitali ya Shanthi ambayo ni ya binafsi Dkt Sanjay Gururaj, amesema kuwa si lazima kwa hospitali za binafsi kutoa ripoti ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo Serikalini.

Related Posts:

  • ZAIDI YA WATOTO 25,000 KUPATA KANSA KILA MWAKA.. Katika Kuadhimisha Siku ya Saratani duniani, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania (FoCC) Janeth Manoni, amesema kwa sasa ugonjwa huo umekuwa tishio kwa watoto nchini, ambapo in… Read More
  • WATU WATANO WAAMBUKIZWA UKIMWI HOSPITALINI CHINA.. Hospitali moja nchini Uchina imekiri kwamba watu watano waliambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi hospitalini humo kimakosa. Waliambukizwa na mhudumu wa afya ambaye alitumia tena vifaa vya matibabu ambavyo vilifaa ku… Read More
  • HIVI NDIVYO DAWA ZA KULEVYA ZINAVYOHARIBU UBONGO. Watafiti wamefanya chunguzi mbalimbali kwa kutumia wanyama kama mfano wa kazi amilifu za ubongo wa binadamu ili kufafanua michakato ya kimsingi ya dawa za kulevya katika ubongo. Mada hii ya kushangaza inashirikisha maeneo… Read More
  • WAGONJWA SASA KUWEKEWA MOYO BANDIA... Nchini Marekani kila baada ya dakika 10 mtu mmoja huwekwa kwenye foleni ya watu wanaosubiri kuwekewa moyo mpya ili kuweza kuendelea kuishi. Hali hii hutokea baada ya moyo wa mgonjwa kuonekana hauwezi kufanyiwa matibabu … Read More
  • VYOMBO VYA PLASTIKI CHANZO CHA SARATANI…. Imebainika kuwa vifaa vya plastiki hutengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200, hivyo kuwa chanzo cha aina 100 za ugonjwa wa saratani. Vifaa hivyo vya plastiki ni pamoja na mifuko ya rambo, bakuli, vikombe na vifaa vya kuhif… Read More

0 comments:

Post a Comment