Tuesday, 29 August 2017

VIDEO: LISSU, LHRC WAUNGANA KUPINGA KULIPULIWA OFISI YA MAWAKILI…………

Tundu Lissu na Kituo cha Haki za Binadamu zimeungana kwa pamoja katika kupinga kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za IMMMA Advocates.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimemtaka Kaimu Jaji Mkuu, Ibrahim Juma kukemea hadharani shambulizi lililofanyika katika ofisi za wanasheria za Immma Advocates.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo­Bisimba amesema tangu kutokea mlipuko usiku wa kuamkia Agosti 26, hakuna kiongozi wa Serikali ambaye amekemea.
Amesema hata kaimu jaji mkuu anayesimamia mhimili wa Mahakama naye amekaa kimya kama vile hakuna tukio lililotokea.
Dk Kijo­Bisimba amesema leo Agosti 29 kuwa, kitendo cha mawakili kuvamiwa kimewatia hofu wanataaluma hao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment