Thursday, 10 August 2017

FACEBOOK KUJA NA RUNINGA YA MTANDAONI..

Kampuni kubwa zaidi ya mitandao ya kijamii duniani Facebook, inatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”watch” ama tazama.

Facebook inasema kwamba imewekeza mamilioni ya dola katika kuufanya mfumo huo kupendwa zaidi.
Teknolojia hiyo imebuniwa ili kushindana na televisheni za kawaida pamoja na mitandao ya you tube Netflix, twitter na snap chat.
Facebook inasema kwamba imewekeza mamilioni ya dola katika kuifanya huduma hiyo kupendwa zaidi.
Nayo Kampuni ya Disney jana ilitangaza kuwa kuanzia mwaka 2019, itafuta makubaliano kati yake na kampuni ya Neflix na kuunda huduma yake mpya ya video.
Facebook tayari ina vipindi kadha vikiwemo vya michezo, vya familia na vya televisheni ya National Geographic.

Watch itaanza kuonyeshwa nchini Marekani kabla ya maeneo mengine kuruhisiwa kutazama.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment