Tuesday 22 August 2017

INDIA YAPIGA MARUFUKU TALAKA YA KUTAMKA TU…

Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake.



India ni moja ya nchi chache ambapo mwanamume muislamu anaweza kumtaliki mkewe kwa kutamka neno talaq mata tatu.
Uamuzi huo wa mahakama unafutia kesi zilizokuwa zikipinga talaka hiyo.
Kesi hizo ziliwasilishwa mahakamani na wanawake watano waislamu, waliokuwa wamepewa talaka kwa njia hiyo pamoja na na makundi mawili ya kutea haki.
Miaka ya hivi karibuni visa vingi vimeibuka ambapo wanaume waislamu huwataliki wake zao kwa kutamka neno talaq mara tatu, kwa njia ya simu au kwa kutuma ujumbe ya sms, kupitia WhatsApp na Skype.


Licha ya njia hiyi ya kutaliki kutumiwa kwa miongo kadha, hiajatajwa popote pale kwenye Sharia au Koran.

0 comments:

Post a Comment