Saturday, 19 August 2017

ZAIDI YA WATOTO 35,000 WAPATA CHANJO YA POLIO SYRIA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO kwa kushirikiana na wadau wengine wamekamilisha duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa polio nchini Syria.

Mashirika hayo yanasema kampeni hiyo imetoa kinga madhubuti dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya 355,000 walio chini ya umri wa miaka mitano katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika ya majimbo ya Deir Ez Zor na Raqqa, ambako machafuko yanayoendelea yamekuwa kikwazo kikubwa.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNICEF Syria Fran Equiza, hakuna mtoto anayestahili kuishi na athari mbaya za polio.
Huu ni mlipuko wa pili wa polio Syria tangu kuanza kwa machafuko 2011 yaliyoathiri sana mfumo wa afya wa nchini humo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment