Thursday, 31 August 2017

WATU MAARUFU WADUKULIWA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM…..

Instagram imegundua dosari katika mfumo wake iliofichua nambari za simu za watu maarufu pamoja na anwani zao kwa wadukuzi wa mitandao.

Mtandao huo unaomilikiwa na Facebook tayari umewasiliana na watu hao ili kuwaelezea dosari iliotokea.
Imesema inaamini kwamba wadukuzi waliwalenga watu maarufu ili kupata habari zao za mawasiliano.
Instagram imesema kuwa nywila hazikuibiwa lakini ikawaonya wateja wake kuchunguza mienendo isiokuwa ya kawaida katika akaunti zao.
Hatahivyo haikutaja ni akaunti za watu gani zilizoathirika.
Dosari hiyo ya kiusalama wa mitandao ilitokea kutokana na tatizo katika programu ya kampuni hiyo.
Hatahivyo imesema kuwa tatizo hilo limeangaziwa.
Kampuni hiyo imewaonya wateja wake kuwa waangalifu kuhusu simu wasizotarajia, ujumbe na barua pepe.

Instagram ina zaidi ya wateja milioni 500 duniani,wateja milioni 300 wanautumia mtandao huo mara moja kwa siku.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment