Thursday 31 August 2017

WANAFUNZI KUFUNZWA KUHUSU NJIA ZA KUTOA TALAKA INDIA…

Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.

Shule ya Dargh-E-Ala Hazrat inayodhibiti madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza hilo kufuatia agizo la mahakama lililopiga marufuku talaka za moja kwa moja.
Wasomi wa Kiislamu wamedai kwamba talaka za moja kwa moja haziambatani na sheria ya kiislamu.
Kiongozi mmoja wa dini kutoka shule hiyo amesema kuwa wataanzisha kifungu kitakachoangazia maswala ya talaka.
Mtaala wa shule hiyo ambao unaangazia Koran na sheria za kiislamu unazungumzia kuhusu talaka lakini sio kwa maelezo ya kina.
Aliongezea kuwa hatua hiyo itaelezea vyema kwamba talaka ya moja kwa moja zinazoetekelezwa nchini India haziambatani na sheria za Kiislamu.
Haijulikani ni umri upi wanafunzi hao wote wakiwa wavulana wenye kati ya miaka mitano hadi 16 watafunza kuhusu talaka.

0 comments:

Post a Comment