Wednesday, 2 August 2017

KAMPUNI YA CHINA YASHTAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA GAMBIA…..

Wanamazingira kutoka miji midogo ya pwani nchini Gambia wameipeleka kampuni moja ya China mahakamani kwa madai ya kutupa takataka za sumu kwenye bahari.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukubaliana nje ya mahakama na kampuni hiyo ya Golden Lead kumaliza tatizo hilo.
Wakazi wa eneo la Gunjur takribani kilimita arobaini kusini mwa mji Mkuu wa Banjul wamesema mamia ya samaki wamekuwa wakifa katika eneo hilo la bahari tangu kampuni hiyo ya Golden Lead ilipojenga kiwanda cha kusindika samaki katika mji huo mwaka 2016.
Wanasema watu ambao wamekuwa wakiogelea katika eneo hilo wamekuwa wakidhurika na kupata matatizo ya kiafya.
Kampuni ya Golden Lead imepinga tuhuma hizo.
Kampuni hiyo ilikubaliana kumaliza suala hilo nje ya mahakama na Mamlaka ya taifa ya Mazingira nchini Gambia mwezi uliopita.


Related Posts:

  • WABUNGE WAIDHINISHA KILIMO CHA BANGI UHOLANZI. Bunge la chini nchini Uholanzi, limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi. Mswada huo ulioidhinishwa utawakinga wakulima wa bangi, ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa. Mswada huo bado haujaidhini… Read More
  • TRUMP AMSHUTUMU OBAMA KUMDUKUA….. Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amegundua Rais mstaafu wa nchi hiyo ambaye ni mtangulizi wake, Barack Obama alikuwa akidukua simu yake mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo. Rais Trump ametoa … Read More
  • NJAA YASABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU 100 SOMALIA... Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizo… Read More
  • MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA AKIWA MAITI.. Grace Mugabe na mumewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti. Bwana Mugabe, ambaye ataku… Read More
  • KASHMIR:MARUFUKU MATUMIZI YA ANASA….. Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa. Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa. Idadi ya aina … Read More

0 comments:

Post a Comment