Thursday, 24 August 2017

MWANAFUNZI AFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI NA DALADALA MOROGORO…

Mtu mmoja amefariki na wawili wamejeruhiwa baada ya gari ya abiria kugonga treni eneo la Tanesco Morogoro.

Akidhibitisha tukio hilo Mganga Mkuu wa hospitali Frank Jacob amesema kwamba, ajali hiyo imetokea leo asubuhi Gari hilo lilikuwa limebeba wanafunzi lilipata ajali eneo la masika baada ya kugonga treni na kuburuzwa umbali wa takriban mita 50 toka yalipo makutano ya reli na barabara.


Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoni humo Ulrich Matei,akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi na imehusisha gari aina ya daladala yenye amba za usajili T 438 iliyokuwa inakwenda Mvumi kwenye njia panda inayoingilia treni.

Kamanda Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni daladala kuingia kwenye njia ya treni bila kusimama ili kuangalia kama kuna treni inakuja, ndipo treni hiyo ikaburuza gari hiyo kwa umbali mrefu na kusababisha maafa hayo.
Msikilize hapa chini kamanda wa polisi mkoani humo Ulrich Matei akielezea tukio hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment