Tuesday, 16 February 2016

RAS LION AMLILIA JOHN WOKA...

Msanii wa muziki wa kizazi kipya John Woka toka kundi la watukutu, amefariki dunia alfajiri ya february 16 katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.


John woka alitamba na ngoma zake kali kama mganga, hii kitu hii na kupendwa na mashabiki kwa style yake ya kurap kama mlevi.

John woka amefariki baada ya kupata ajali wakati anatengeneza gari maeneo ya sinza katika mfumo wa Ac.

Inasemekana kuna kitu kilivyetuka baada ya kufungua Ac na kumpiga kwenye paji la uso na kuingia kama nchi 3 au 2 na kusababisha damu nyingi kumwagia ndani ya kichwa.

Mpaka alipofikishwa hospitali ya muhimbili Woka alikuwa katika chumba cha ICU, na hali yake ilikuwa mbaya mpaka alipoaga dunia alfajiri ya tarehe 16 february 2016.

Bonyeza Play hapa chini kumsika kile ambacho amekizungumza Ras Lion ambaye alikuwa mtu wa karibu kabisa na John woka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment