Maeneo mengi
ya Uchina hasa miji mikubwa, yamekuwa yakitatizwa na uchafuzi wa hewa.
Leo De Watts 27 hutoa hewa yake maeneo ya mashambani
Uingereza, ambayo hayajachafuliwa na kuipakia kwenye chupa na kuisafirisha hadi
miji ya Shanghai na Beijing, na kuwauzia matajiri hewa hiyo.
Chupa moja ya
hewa hiyo safi ya mililita 580 huwa anauza £80 ($115).
Kutokana an biashara hiyo ameanzisha kampuni kwa jina Aethaer,
na hutoa hewa yake maeneo yenye upepo mwingi ya Dorset, Somerset, na Wales.
Anasema baadhi ya wateja hutaka hewa ya kiwango Fulani, na
wakati mwingine humbidi kutoa hewa maeneo ya milima, na wakati mwingine bondeni
ili kupata aina ya hewa inayohitajika na wateja wake.
Linaonekana kama wazo la kushangaza sana hapa kwetu sababu
tuna hewa safi, lakini huko kwawenzetu hakuna hewa safi na inathaminiwa sana.
Viwango vya uchafuzi wa hewa Uchina vilifikia viwango vya juu sana,
hasa mwezi Desemba, na katika baadhi
ya maeneo kusababisha shule kufungwa.
Lakini Watts si
mtu wa kwanza kuuza hewa nchini China, kwani kunao wafanya biashara ambao
wamekuwa wakiuza hewa safi kutoka nchini kama vile Canada.
0 comments:
Post a Comment