Kampuni
moja ya India inatarajiwa kuzindua kile kinachojulikana kuwa simu aina ya
smartphone ya bei rahisi.
Kampuni ya Ringing Bells imesema
kuwa simu hiyo kwa jina Freedom 251 itagharimu Rupee 500 sawa na dola
7.3,lakini vyombo vya habari nchini India vimesema kuwa itauzwa kwa Rupee 251
pekee ambazo ni sawa na dola 3.67.
Ripoti zinasema simu hiyo ina
ukubwa wa 8GB na ina kamera mbele na nyuma.
India ni soko la pili kwa ukubwa
la simu na lina wateja bilioni moja wanaomiliki simu.
Freedom 251 inatarajiwa kulenga
soko ambalo tayari linatawaliwa na simu za bei ya chini.
Hii ndio modeli yetu ya kwanza na tunafikiri kwamba
inaleta mabadiliko katika soko la simu, shirika la habari la AFP, lilimnukuu
msemaji wa kampuni hiyo akisema.
Kwa sasa kampuni hiyo inanunua
vifaa vya kutengezea simu kutoka nje kabla ya kuviunganisha nchini India, lakini
ina mpango wa kutengeza vifaa hivyo nchini India katika kipindi cha mwaka mmoja
ujao,aliongezea.
Kampuni ya Ringing Bells
ilianzishwa miezi michache iliopita na hivi majuzi ilizindua simu ya be rahisi
ya smartphone inayotumia mtandao wa 4G inayouzwa Rupee 2,999, chombo cha habari
cha Press Trust kiliarifu.
0 comments:
Post a Comment