Mamilioni ya watu wenye asili ya China
duniani kote, wanasheherekea mwaka mpya wa ki China.
Baruti
nyingi zilirushwa angani mjini Beijing, ikiwa ni ishara ya kusheherekea siku ya
kwanza ya mwaka mpya wa nyani nchini nhumo.
Nyani ni miongoni
mwa wanyama kumi na mbili wanaotumiwa kati ya alama za kichina katika masuala
ya utabiri.
Nako
mjini Yokohama nchini Japan wao wanasheherekea siku kuu hii kwa kuhesabu muda
huku wakicheza ngoma ya asili ya kucheza na simba.
Maadhimisho
ya sherehe hizi za mwaka mpya zinajumuisha watu kula pamoja,kufanya usafi na
familia kuwa pamoja huku wakirusha fashi fashi angani.
0 comments:
Post a Comment