Takwimu rasmi ya idadi ya watu nchini Japan,
imeashiria kuwa idadi ya watu nchini humo ilipungua kwa takriban watu milioni
moja katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Hii ni
mara ya kwanza kwa idadi ya watu nchini humo kushuka tangu mwaka wa 1920, licha
ya kuwa wataalamu walikuwa wamebashiri kutokea kwa hali hiyo miongo kadhaa
iliyopita, wakisema kuwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na kutokuwepo
kwa watu wanaoingia nchini humo kuishi.
Tatizo
hilo linatarajiwa kuwa mbale zaidi, utafiti uliofanywa na taasisi inayohusika
na masuala ya sensa , umebainisha kuwa asilimia arobaini ya raia wa Japan
watakuwa na umri wa miaka sitini na tano au zaidi ifikiapo mwaka wa 2050, na
hivyo kuzua wasi wasi kuwa gharama ya kuwatunza watu wakongwe nchini humo
itapanda zaidi.
0 comments:
Post a Comment