Utafiti mpya unaonyesha
kuwa mwanya kati ya matajiri na masikini unazidi kupanuka nchini
Marekani.
Gazeti la Wall-Street
Journal limechapisha ripoti inayoonyesha kuwa, mlingano wa kijamii unazidi
kutokomea miongoni mwa Wamarekani, ambapo Masikini wanazidi kuelemewa nao
matajiri wanazidi kujilimbikizia mali kila uchao.
Utafiti huo mpya
umefichua kuwa, jamii ya Wamarekani weusi imezidi kutengwa na kunyimwa nafasi
sawa na wenzao weupe, jambo linalozidi kupanua pengo kati ya matajiri na
masikini.
Utafiti huo umetumia
vigezo vya afya, ajira na umri wa kuishi watu ili kuandaa ripoti hiyo mpya.
Kwa mujibu wa watafiti huo
ni kwamba,Marekani inaongoza kwa kuwa na ukosefu wa usawa katika jamii.
Ripoti hiyo
imewanyooshea kidole cha lawama wanasiasa wa Marekani, ambapo wanatuhumiwa
kuharibu mazingira ya uwekezaji na hivyo kuongeza kiwango cha ukosefu wa ajira.
Matokeo yake ni kupanuka
mwanya kati ya watu masikini na wale matajiri, katika nchi hiyo inayohesabiwa
kuwa na uchumi mkubwa zaidi duniani.
0 comments:
Post a Comment