Mwalimu mmoja kutoka Kenya ni miongoni
mwa walimu wengine kumi waliofuzu fainali ya
waliorodheshwa, kuwania tuzo ya
mwalimu bora katika harakati zake za kukabiliana na itikadi kali.
Ayub
Mohammed ni mwalimu wa somo la biashara na lile la dini la IRE, katika shule ya
upili ya Eastleigh mjini Nairobi.
Tuzo
hiyo ya dunia ilioanzishwa na hazina ya fedha ya Verkey, ikiwa ni shirika la
hisani la kampuni ya kimataifa ya elimu ya Gems, inayolenga kutafuta habari za
mashujaa wanaobadilisha maisha ya vijana.
Amekuwa akijenga
mtandao wa walimu walio na maono kama yake, na kutengeza utaratibu unaolenga
kukabiliana na itikadi kali.
Tuzo
hiyo ilipata maombi kutoka kwa walimu katika mataifa 148.
Mshindi
ambaye atatangazwa mwezi Machi atapokea dola milioni moja.
Walioorodheshwa
ni pamoja na Aqeela Asifi ambaye anawafunza wakimbizi nchini Pakistan na Hana
Al Hroub, ambaye alilelewa katika kambi moja ya wakimbzi nchini Palestina na
ambaye sasa ni mwalimu.
Mshindi wa tuzo hiyo
mwaka jana alikuwa Ancie Atwell kutoka Marekani, ambaye alitoa fedha hizo kwa
shule yake.
Tuzo
hizo zilitolewa katika sherehe iliohudhuriwa na aliyekuwa rais wa Marekani Bill
Clinton huku Bill Gates akitoa mchango wake.
0 comments:
Post a Comment