Kampuni
ya kutengeneza simu ya Samsung imezindua simu yake mpya ya kisasa aina ya
Galaxy S7
na Galaxy S7 Edge.
Kampuni hiyo ya kutokea Korea
Kusini imezindua simu hizo mbili, ilikukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa
kampuni ya simu ya Apple.
Simu hizo za Galaxy S7
zimerejeshewa uwezo wa kusoma kadi ya kuhifadhia data al maarufu (MicroSD card)
Kikubwa kitenolojia katika simu
hizo mpya za Galaxy S7 ni kuwa zinaweza kutumika hata ndani ya maji bila ya
kuharibika.
Vile vile Galaxy S7 zina
programmu iliyoimarishwa zaidi mbali na kuwa na kamera ya nyuma yenye uwezo wa
kupiga picha hata kwenye mazingira yenye giza totoro na picha hizo zikaonekana
bora.
Wadadisi wa maswala ya teknolojia
hata hivyo hawaoni tofauti kubwa kimsingi kati ya simu hiyo ya Galaxy S7 na ile
ya awali ya Galaxy S6.
Hilo ndilo litakalowasumbua
wauzaji wa simu hiyo mpya kwani umbo na ukubwa wake ni sawasawa na ile ya
Galaxy S6.
Samsung huwa haitangazi idadio ya
simu ilizouza.
Hata hivyo idadi ya mauzo ya
kampuni hiyo ilizorota kwa asilimia 2% katika mwaka wa 2015.
Wapinzani wake wakuu Apple,
Huawei na Xiaomi hata hivyo walisajili kuimarika kwa faida zaidi.
Takwimu ya kampuni moja ya mauzo
ya teknolojia IDC inaonesha kuwa kampuni hiyo ya Korea Kusini ni bora zaidi
katika mauzo ya simu katika vitengo tofauti kote duniani.
Simu hiyo mpya ya Galaxy S7
inaurefu wa nchi 5.5in (14cm).
Simu ya awali ya Galaxy S6
inaurefu wa nchi 5.1 (13cm)
0 comments:
Post a Comment