Mashabiki
wa kilabu Trabzonspor wamefanya maandamano, wakimuunga mkono mchezaji mmoja
ambaye alipewa kadi nyekundu kwa kumuonyesha kadi nyekundi refa.
Salih Dursun alibeba kadi
nyekundu na kumuonyesha refa Deniz Bitnel, na kuwa mchezaji wa nne wa
Trabzonspor kutolewa nje katika mpambano aambao kilabu hiyo ilishindwa 2-1 na
Galatasaray.
Hatahivyo amepata ufuasi kwa
hatua yake, huku Bitnel akikosolewa kwa mchezo wake.
Trabzonspor pia imeanza kuuza
fulana,zinazomuonyesha Dursun akifanya kitendo hicho.
Kumekuwa na ripoti kwamba maafisa wa kilabu hiyo huko
Macka, wanapanga kujenga sanamu ya mchezaji huyo ili kuunga mkono kitendo
chake.
Na huku mashabiki wa kilabu hiyo
wakibeba kadi nyekundu wakiandamana huko Trabzon, mashabiki katika jimbo la
magharibi la Koceli wamewasilisha malalamishi ya uhalifu kwa utumizi m'baya wa
mamlaka na kuchochea chuki.
Tranzospor walikuwa chini na
wachezaji tisa huku ikiwa mabao ni 1-1 wakati refa Bitnel alipompatia kadi
nyekundu Luis Cavandi, kwa kucheza visivyo mbali na kuizawadi Galatasaray
mkwaju wa penalti.
Wakati wa maandamano hayo dhidi ya refa
uwanjani, kadi hiyo nyekundu ilianguka kabla ya Dursun kuiokota na kumuonyesha
refa,ambaye alimpokonya mchezaji huyo na kumuonyesha vilevile hatua
iliosababisha mchezaji huyo kuondoka uwanjani.
0 comments:
Post a Comment