Kuna viwango
vya sukari ya juu vinavyoshangaza, katika vinywaji vya moto vinavyouzwa katika
migahawa kundi moja limeonya.
Kundi hilo limesema kuwa kuna vinywaji 131 vilivyokolea
sukari, huku likifichua kwamba theluthi moja ya vinjwaji hivyo vina sukari
zaidi ya Soda za Pepsi na Coca- Cola ambazo zina vijiko tisa vya sukari.
Shirika hilo la hisani limesema kuwa katika visa vibaya
zaidi,vinywaji hivyo vina zaidi ya vijiko ishirini vya sukari.
Migahawa ya kuuza chai kama vile Starbucks, Costa na Caffe
Nero, vimesema kuwa viko tayari kupunguza sukari katika vinywaji vyao.
Professa Graham Mac Gregor ambaye ni mwenyekiti wa vita dhidi
ya Sukari, amesema ni mfano mwengine wa kashfa ya viwango vya sukari katika
vyakula vyetu na vinywaji.
Vinywaji vilivyochunguzwa ni pamoja
na kahawa kama vile Mochas na Lattes,vinywaji vya matunda, vile vya chokoleti
kutoka kwa maduka ya kahawa na maduka ya kuuza vya kula vya milolongo.
Shirika hilo lilibaini kwamba
asilimia 98 ya vinywaji vilivyopimwa, vitaorodheshwa kama vinywaji vyenye
sukari nyingi.
Kiwango cha sukari kinachohitajika
kwa siku miongoni mwa watu walio juu ya umri wa miaka 11 ni gramu 30 au vijiko
sita, huduma ya kitaifa ya afya imesema nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment