Viongozi
wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi
hizo mbili.
Mkutano huo ndio wa pili kati ya
rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un.
Unafanyika wakati pande hizo
zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea
Kaskazini na Kusini.
Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani
Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini
baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika.
Mazungumzo hayo yalifanyika upande
wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom.
Bw Moon atatangaza matokeo ya
mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi.
Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim
ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka
rasi ya Korea na kumaliza misukosuko.
0 comments:
Post a Comment