This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday 22 April 2013

Kwa nini binadamu hulia?Fahamu sasa..

 

 

 

Wanawake na wanaume hulia tofauti..

Watafiti wa  nchini Ujerumani walifanya utafiti kuhusu kulia na kubaini kuwa wanawake hulia kati ya mara 30 hadi 63 kwa mwaka na wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka.


Wanaume hulia kwa dakika mbili hadi nne wakati wanawake hulia kwa zaidi ya dakika sita.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Kitila Mkumbo anasema kitendo cha kulia kinatokana na mifumo ya hisia.
Anasema binadamu huweza kulia kutokana na hasira, maumivu au furaha.
Zipo aina tatu za machozi
Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yasiathiriwe na vumbi na vitu vingine.
Mirija hiyo ipo chini ya kope za juu na huzalisha maji yenye chumvichumvi ambayo ndiyo machozi-hayo  husambazwa katika jicho- kila  binadamu anapopepesa.
Wanasayansi wanasema, zipo aina tatu za machozi ambazo huzalishwa na macho ya binadamu.
Yapo machozi yajulikanayo kama ‘Basal’ au Basali. Machozi haya yana kazi kubwa ya kulinda jicho na kulipa unyevu.
Machozi mengine ni ya ‘Reflex’ haya yana kazi kubwa ya kutoa tahadhari kwa jicho pale linapoumia. Kwa mfano mtu akikata kitunguu au mdudu akiingia jichoni.
Machozi ya hisia au  ‘Pysch’ haya hutiririka pale ambapo binadamu hupatwa na uchungu, maumivu, msongo wa mawazo au furaha.
Tafiti zinaonyesha kuwa machozi ya hisia yana kiwango cha manganizi, chembechembe ambazo huathiri tabia au roho ya binadamu.
Machozi hayo ya hisia pia yana vichocheo vya prolactini ambavyo husimamia uzalishwaji wa maziwa.
Machozi yanayozalishwa kwa hisia yana mchanganyiko wa kemikali tofauti na aina nyingine za machozi.


Hivyo basi, binadamu anapolia, hutoa manganizi, potashiam na prolactini.
Chembechembe hizo zinatajwa kupunguza mshtuko au huzuni kwa  kuweka uwiano wa msongo wa mawazo katika mwili.

Sunday 14 April 2013

Hatari:Aina Mpya ya Kisonono Yasambaa Duniani

ina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa (resistant to drugs) zinazotumika kutibu ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema, ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa.
Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono kuwa na athari nyingi kama mcharuko (inflammation), ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama wajawazito.
“Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu dhidhi ya dawa zote za antibiotiki tunazotumia dhidhi yake ikiwemo dawa za jamii ya cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono, “ alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan, mmoja wa wanasayansi wa shirika la afya duniani katika kitengo cha magonjwa ya zinaa.
Miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidhi ya dawa zote ambazo tunazo saizi “aliendelea kusema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan wakati wa mahojiano na shirika la habari la The Associated Press kabla WHO haijatangaza rasmi hatua na mwongozo mpya wa kukabiliana na tishio la aina hii mpya ya kisonono.
Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi (VVU).
“Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,’” alinukuliwa akisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.
Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidhi ya dawa aina ya cephalosporins  viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway.
Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa sasa duniani bila kuweza kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu  mzuri wa wagonjwa wake.
Shirika la afya duniani limesema nchi zinatakiwa kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.
“Elimu ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya kondomu inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono. Hatuwezi kuutokomeza kabisa ugonjwa huu bali tunaweza kuzuia usambaaji wake,”alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.

Protini Yagundulika Kusababisha Saratani ya Matiti kwa Wanawake Wanaotumia Vilevi

Kimengenyo (enzyme) ambacho ni protini aina ya CYP2E1 kimegundulika kuwa ndio chanzo kinachochangia wanawake kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia vilevi. Kwa muda mrefu wanasayansi walikuwa wakitafuta uthibitisho wa uhusiano wa kunywa pombe na saratani ya matiti, lakini sasa wameweza kupata uhusiano huo. Protini hii hupatikana kwenye matiti ya wanawake na hivyo kuwaweka kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti kama watakuwa wanakunywa sana vilevi kama pombe, whiskey, wine na nk.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Autonomous University of the State of Morelos cha nchini Mexico, umeonyesha ya kwamba protini hiyo ya aina ya CYP2E1 inauwezo wa kukivunja vunja kilewesho (ethanol) na kusababisha kutolewa kwa kemikali hatari zinazojulikana kama free radicals.
Watafiti hao wamesema ugunduzi wao utasaidia katika kuvumbua kipimo kitakachosaidia kujua ni wanawake gani walio na protini hii ya CYP2E1 na hivyo kuwasaidia kujikinga dhidhi ya saratani ya matiti.
Kemikali hizi hatari uhusishwa na kutokea kwa baadhi ya magonjwa kama saratani mbalimbali, ugonjwa wa kisukari, uharibifu wa mishipa ya damu aina ya ateri (arteries), kuchangia mtu kuzeeka na nk.
Swali kuu walilojiuliza watafiti wakati wa utafiti huo ni , Je kuwa na protini hii ya CYP2E1 kwa wingi huchangia mwanamke kupata ethanol-induced toxicity na hivyo kumhatarisha kupata saratani ya matiti?
Matokeo yetu yalionyesha ya kwamba seli za kutoka katika matiti ya mwanamke (mammary cells) zilizowekwa kilewesho cha aina ya ethanol, hutoa kemikali hatari kwa wingi, husababisha kuwepo kwa oxidative stress, huharakisha ufanyaji kazi wa seli na hivyo kuongeza kiwango cha ukuaji wa seli hizi kwa wingi na kusababisha saratani ya matiti” alisema Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso, kutoka chuo kikuu cha The Autonomous University of the State of Morelos cha nchini Mexico.
“Kama wewe ni mwanamke ambaye una kiwango kikubwa cha protini hii ya CYP2E1 katika matiti yako na unakunywa pombe basi utakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na mwanamke ambaye ana kiwango kidogo cha protini hii katika matiti yake.” Aliendelea kusema Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso.
Uchunguzi uliofanywa kutoka kwenye tishu za matiti ya wanawake wenye afya njema ambao wamefanyiwa upasuaji wa kukuza matiti yao umeonyesha viwango tofauti vya protini hii katika wanawake hawa.
“Hii inamaanisha ya kwamba wanawake wanatafautiana kwa umengenywaji wa pombe na hivyo inabidi kila mwanamke kuchukua hatua tofauti katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti” Alisema tena Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso.
Protini hii ya aina ya CYP2E1 hupatikana katika seli za matiti ya mwanamke zinazojulikana kama mammary epithelial cells ambapo pia ndio chanzo cha seli/chembechembe nyingi za saratani ya matiti na kusababisha watafiti hao kuanza kushuku uhusiano wake na saratani ya matiti.
Ili kuthibitisha shauku yao kwamba protini hii husababisha saratani ya matiti, watafiti hao walichukua tishu za matiti zilizo na viwango tofauti vya CYP2E1 na kuziweka kwenye pombe. Matokeo yalionyesha ya kwamba seli zenye kiwango kidogo cha protini aina ya CYP2E1 hazikuathiriwa sana ikilinganishwa na seli ambazo zilikuwa na kiwango kikubwa cha protini hiyo.
Utafiti huu ni ushindi mkubwa katika vita dhidhi ya saratani ya matiti kwani utasaidia kupunguza kiwango cha saratani hii kwa wanawake

Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?

Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani  umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).
Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit) pekee kwa  mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi  Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
 
Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha  East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
 
Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha  miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids - flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.
 
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha  25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu.
 
Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
 
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
 
Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata  kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).
 
 
Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
 
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula  kiwango kikubwa cha antioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.
 
Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.
 
Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi),kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya  kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya  kutosha na kupunguza msongo wa mawazo. 


Friday 12 April 2013

Upara,sababu ya maradhi ya moyo?....



Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani.
Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.
Utafiti huu uliowahusisha watu elfu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.

Hata hivyo watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.

Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapaswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.

Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume .

Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.

Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na maradhi ya moyo.

Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo.

Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.

Daktari Tomohide Yamada wa chuo kikuu cha Tokyo,amesema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo.

Amesema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo

Aidha amesema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.

Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.

Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.

Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.

Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.