Monday, 22 April 2013

Kwa nini binadamu hulia?Fahamu sasa..

 

 

 

Wanawake na wanaume hulia tofauti..

Watafiti wa  nchini Ujerumani walifanya utafiti kuhusu kulia na kubaini kuwa wanawake hulia kati ya mara 30 hadi 63 kwa mwaka na wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka.


Wanaume hulia kwa dakika mbili hadi nne wakati wanawake hulia kwa zaidi ya dakika sita.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Kitila Mkumbo anasema kitendo cha kulia kinatokana na mifumo ya hisia.
Anasema binadamu huweza kulia kutokana na hasira, maumivu au furaha.
Zipo aina tatu za machozi
Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yasiathiriwe na vumbi na vitu vingine.
Mirija hiyo ipo chini ya kope za juu na huzalisha maji yenye chumvichumvi ambayo ndiyo machozi-hayo  husambazwa katika jicho- kila  binadamu anapopepesa.
Wanasayansi wanasema, zipo aina tatu za machozi ambazo huzalishwa na macho ya binadamu.
Yapo machozi yajulikanayo kama ‘Basal’ au Basali. Machozi haya yana kazi kubwa ya kulinda jicho na kulipa unyevu.
Machozi mengine ni ya ‘Reflex’ haya yana kazi kubwa ya kutoa tahadhari kwa jicho pale linapoumia. Kwa mfano mtu akikata kitunguu au mdudu akiingia jichoni.
Machozi ya hisia au  ‘Pysch’ haya hutiririka pale ambapo binadamu hupatwa na uchungu, maumivu, msongo wa mawazo au furaha.
Tafiti zinaonyesha kuwa machozi ya hisia yana kiwango cha manganizi, chembechembe ambazo huathiri tabia au roho ya binadamu.
Machozi hayo ya hisia pia yana vichocheo vya prolactini ambavyo husimamia uzalishwaji wa maziwa.
Machozi yanayozalishwa kwa hisia yana mchanganyiko wa kemikali tofauti na aina nyingine za machozi.


Hivyo basi, binadamu anapolia, hutoa manganizi, potashiam na prolactini.
Chembechembe hizo zinatajwa kupunguza mshtuko au huzuni kwa  kuweka uwiano wa msongo wa mawazo katika mwili.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment