Raia mmoja wa Marekani anayefanya kazi katika mataifa ya milki za kiarabu UAE, amekamatwa kwa matamshi aliyochapisha katika mtandao wake wa facebook na sasa anakabiliwa na hukumu ya kufungwa jela. Ryan Pate ambaye ni fundi wa ndege,alikuwa katika likizo ya kujiuguza nyumbani kwake katika jimbo la Florida nchini Marekani wakati alipomkosoa mwajiri wake. Aliita kampuni hiyo kama yenye ''wasaliti na kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu wa mataifa ya milki hiyo. Wakati alipokuwa akirudi alikamatwa kwa kukiuka sheria kali za taifa hilo kuhusu matamshi ya kashfa. Iwapo atapatikana na hatia huenda akahudumia kifungo cha hadi miaka mitano jela.
MHE. NDERIANANGA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS IFAD
-
NA. MWANDISHI WETU BERLIN, UJERUMANI
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na
Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekut...
1 day ago
0 comments:
Post a Comment