Tuesday 17 March 2015

Harufu ya Choo yalazimu ndege Kutuaa dakika chache baada ya kuruka..!!

Ndege moja ya shirika la ndege la British Airways,ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai,imelazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea kwenye choo.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo bwana Abhishek Sachdev,aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa ''Amini usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu
kugundua kuwa harufu mbaya inatokea kwenye choo cha ndege hiyo.''
Yamkini rubani wa ndege hiyo alimwita msimamizi wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo tukang'amua kuwa kulikuwa na tashwishi katika safari yetu''Sachdev alinukuliwa na gazeti moja.
''Kufikia wakati huo ilikuwa ni takriban nusu saa tangu tupae angani kwa hivyo tukalazimika kurejea Dubai''
Mwakilishi wa ndege hiyo Greg James, Sarah, aliiambia Radio moja kuwa hilo halikuwa swala la kufanyiwa utani kwani ukiwa ndani ya ndege ni tishio kubwa kwa afya ya rubani na abiria kwa jumla.

Ndani ya ndege huwa kunautupu wa hewa kwa hivyo asili mia 50 ya hewa inayotumika ni ileile kwa hivyo harufu mbaya ingeathiri vibaya afya ya abiria ndio sababu ndege hiyo haikuwa na budi ila kurejea ili isafishwe.
Hata hivyo shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa usumbufu wowote kwa abiria wake walioathirika siku hiyo.

0 comments:

Post a Comment