Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Maliasili nchini Kenya Richard Lusiambe
(wakwanza kulia) akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki
nchini Tanzania Gladness Mkamba mara baada ya kutia saini makubaliano ya
Tanzania na Kenya kupiga vita biashara haramu ya mbao pamoja na mazao ya misitu
inayofanyika kupitia mipaka ya nchi hizo katika mkutano uliofanyika jijini
Arusha.
Makubaliano
hayo yamefanyika hii leo jijini Arusha mbele ya wakurugenzi na wataalamu
mbalimbali wa masuala ya maliasili na misitu kutoka nchini Kenya na Tanzania
katika ukumbi wa mikutano wa Naura Hotel.
Serikali
ya kenya imeishukuru Tanzania kwa kusaini makubaliano hayo na kuahidi kulinda
misitu ambayo imepakana na Tanzania pamoja na kukabiliana na uhalifu unaofanywa
na majangili.
Akizungumza
katika makubaliano hayo katibu mkuu wa wizara ya mazingira nchini Kenya Richard
Lisyambe,amesema kila mwaka zaidi ya
dola 15 zinapotea kwa ajili ya kukabiliana na wawindaji haramu na wanaofanya
biashara ya bidhaa zitokanazo na na misitu kinyume na sheria.
Amesema
kuwa asilimia 65 ya wananchi wa Kenya wanatumia mkaa hali ambayo inachangia
uharibifu wa misitu huku akieleza kuwa watahakikisha wanapunguza kwa kiasi
kikubwa matumizi ya mkaa kwa kutoa elimu kwa wananchi nchini humo.
Kwa
upande wake afisa misitu Tanzania Juma Mgoo amesema kuwa huu ndio muda wa
wananchi kuelewa umuhimu wa mali asili na misitu na kuahidi kusimamia ipasavyo
na kusema kuwa watahakikisha wanawachukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote
atakaebainika kufanya uharibifu wowote wa mazingiara.
Makubaliano
haya yamekuja ikiwa nchi zote mbili Tanzania na Kenya zipo katika vita kubwa ya
kukabiliana na majangili ambao wanatishia kutoweka kwa maliasili zilizopo ikiwa
ni pamoja na wanyamapori.
0 comments:
Post a Comment