Wednesday 25 March 2015

Awaua wanawe na kuwaweka ndani ya Jokofu



 
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamke huyo mama wa watoto wanne,aliwatumbukiza wanawe wawili wenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye umri wa miaka 14 ndani ya jokofu baada ya kuwaua.
Miili hiyo ilipatikana na maafisa wa idara ya mahakama waliokwenda nyumbani kwa mama huyo,kwa nia ya kumfurusha baada ya kushindwa kugharamia kodi ya nyumba .
Walishtuka kupata miili ya watoto hao na mara moja wakawaarifu maafisa wa polisi katika jimbo hilo.
Uchunguzi na upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika ilikubaina kiini haswa cha vifo vyao.
Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo James Craig,ametaja kitendo cha mwanamke huyo kuwa cha kuogofya mno.
Majirani wengine walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa taabani haswa,baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, na kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 36,alikuwa kanakwamba anakabiliwa na upungufu fulani maishani mwake.

0 comments:

Post a Comment