Monday 16 March 2015

Under 18 Uingereza kufunzwa Somo kuhusu ubakaji....

Wanafunzi kuanzia miaka 11 nchini Uingereza watafundishwa kuhusu tofauti kati ya ubakaji na tendo la ngono ambalo limetekelezwa kutokana na idhini ya wapenzi wawili kama mojawapo ya mipango ya kuwawapa ujuzi kuhusu maisha ya sasa nchini humo
Somo hilo ambalo litaanzishwa mara moja baada ya siku kuu ya Easter litaongezwa katika mtaala wa Uingereza baada ya wasiwasi kutolewa kwamba vijana walikuwa wakishinikizwa kushiriki katika ngono.
Nick Morgan ambaye ni katibu wa elimu alitoa tangazo hilo siku ya kimataifa ya wanawake.
''Lazima swala hili tulikabili kwamba mambo ambayo wasichana wetu wanapitia hayakuwepo wakati wa ujana weyu,kwa hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wasichana wetu wanamaliza shule wakiwa na uwezo wa kukabiliana na changaomoto watakazokumbana nazo wakiwa watu wazima'', aliandika.

0 comments:

Post a Comment