Friday, 27 March 2015

TAFITI:Kilimanjaro vinara wa kunywa viroba..!!!!



Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe  hasa ya  viroba,
ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.
Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa Matumizi ya Pombe kwa vijana  katika mikoa ya  Kilimanjaro, Mwanza, Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza  kwa unywaji wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo.
Akitoa matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la  ripoti ya utafiti wa ukubwa wa matumizi ya pombe nchi, Mtafiti wa NIMR Dk  Saidi Kapiga  amesema  hapa nchini matumizi ya pombe ni makubwa na wanaume wanaongoza kwa kunywaji wa pombe kuliko wanawake licha ya  kuwa na madhara kwa watumiaji.
Utafiti wa Mwanza, Geita na Kahama
Alisema utafiti uliofanywa na NIMR katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kahama kwa kipindi cha mwaka jana ulibaini wanaume wanaongoza, kwani kati ya watu wazima 1000 tuliowauliza juu ya matumizi ya pombe, asilimia 28.5 ya wanaume na wanawake asilimia 13.
Mtafiti wa Sayansi ya Jamii kutoka kituo cha NIMR mkoani Mwanza, Haika Osaki amesema utafiti waliofanya katika Mkoa wa Kilimanjaro ulihusisha matumizi ya pombe aina ya viroba.
Osaka alisema walishirikisha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kutoka katika makundi ya  shule,vyuo na vibarua ambapo utafiti ulibaini kuwa vijana wengi wanajiusiha na matumizi ya pombe kali aina ya viroba kutokana na bei ndogo ya bidhaa hiyo.

0 comments:

Post a Comment