Friday 13 March 2015

Idadi ya mimba za utotoni yaongezeka..!!!!!

Msichana mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka 15 hadi 19 ni mjamzito au ana mtoto imeelezwa. Idadi hii inawakilisha maisha halisi na kuonesha kwamba kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa, wasichana wataendelea kukosa haki zao za msingi na kuzidi kuwa wategemezi. Hayo yalisema na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa utafiti katika ukunga, ulioandaliwa na LUGINA Afrika Midwives Research Network (LAMRN) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),amesema vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano,ni tatizo katika nchi zote zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika hata hivyo jitihada mbalimbali zinafanyika ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua au kumalizika kabisa. Kuhusu mimba za utotoni Mwenyekiti huyo wa WAMA, amesema tafiti zilizofanyika zinaonesha wasichana wanaanza kufanya mapenzi mapema zaidi wakiwa na umri mdogo, ukilinganisha na wavulana jambo linalopelekea kupata mimba za utotoni na hivyo kukosa elimu kwa kukatisha masomo yao

0 comments:

Post a Comment