Tuesday 17 March 2015

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry kuondoka jeshini Juni..

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry amesema anaangalia mustakhabali mwingine wa maisha baada ya kuthibitika kuwa ataacha jeshi mwezi Juni.
Taarifa kutoka makazi ya kifalme ya Kensington imesema Prince Harry atamaliza utumishi wake wa miaka kumi jeshini baada ya wiki nne kwenda kutumikia katika jeshi la ulinzi la Australia, kuanzia mwezi April.
Mrithi wa nne katika mfuatano wa warithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza amesema uzoefu wake jeshini utabakia katika maisha yake yote.

Prince Harry amesema bado alikuwa akitafakari ajira yake.
Prince Harry ameshiriki mapigano mara mbili nchini Afghanistan, vita vya karibuni kabisa ni pale aliposhiriki mwaka 2012 akiwa rubani wa helikopta ya kijeshi aina ya Apache.
Prince Harry ametajwa kuwa rubani aliyetoa msaada mkubwa kwa wapiganaji wa ardhini kwa kuwajali.

0 comments:

Post a Comment