Utashi wa kisiasa upo ili kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino,amesema Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, baada ya Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuziomba serikali za Tanzania, Malawi na Burundi kuchukua hatua za kusitisha mauaji hayo. Bi Chana amesema hatua ya kwanza itakayochukuliwa na serikali ya Tanzania ni kuwapatia wahalifu wa mauaji hayo adhabu kali, ikiwemo hukumu ya kifo, hata kama Tanzania haijatekeleza adhabu hiyo kwa muda mrefu. Kadhalika amesema kama nchi nyingine zinzvyochukua hatua dhidi ya ugaidi, serikalia ya Tanzania ina haki ya kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya mauajia ya albino. Hatimaye ametoa wito kwa watanzania wote waonyeshe ubinadamu na huruma ili kukomesha ukatili huo ambao ni kinyume na haki za binadamu.
TANZANIA,JICA KUPANUA USHIRIKIANO KWENYE UTAFITI WA MADINI MUHIMU NA
KIMKAKATI
-
-Zaidi ya Wataalamu 30 Wanufaika na mafunzo kupitia Mradi wa Kizuna
📍 Dodoma
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini na Shirika la Ushirikiano wa...
3 hours ago







0 comments:
Post a Comment