Mwandishi maarufu wa runinga kutoka Afrika Kusini ameibiwa hadharani alipokuwa akijiandaa kwenda hewani mbele ya kamera. Kanda ya video imewaonyesha wanaume wawili wakimvamia Vuyo Mvoko, kutoka yuninga ya taifa ya SABC ambaye alikuwa nje ya hospitali moja ya mjini Johannesburg akiripoti kuwasili kwa rais wa Zambia ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu. Bwana Mvoko baadaye alisema kuwa mmoja wa wezi hao alimtishia na bunduki alipokataa kumpa simu yake ya rununu. Wezi hao walionekana kutojali kamera zilizokuwa mbele yao. ''Sikuelewa ni kwa nini waliweza kunivamia mbele ya Kamera ilihali taa zote zilikuwa zikiwaka na kamera zilikuwa zikinasa kila kitu na, waliona kilichokuwa kikiendelea''. Baada ya mda mfupi bwana Mvoko ambaye ni mhariri wa kituo hicho cha habari alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa yuko salama salmin na kutuma kanda ya video hiyo mtandaoni. Maafisa wa polisi wanasema kuwa wezi hao waliiba laptopu, na simu na kwamba maafisa walikuwa tayari wanachunguza kisa hicho.
SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA VYAKULA VYA ASILI KUIMARISHA AFYA NA KUZUIA
MAGONJWA
-
Na Elimu ya Afya kwa Umma
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewahimiza Watanzania kurejea katika
matumizi ya vyakula vya asili kama sehemu muhimu ya kuje...
1 hour ago







0 comments:
Post a Comment