Chama
cha walimu wilaya ya MISENYI mkoani Kagera wanatarajia kuitisha mgomo
usiokuwa na kikomo kwa kutofundisha katika shule za msingi na sekondari
endapo uongozi wa halmashauri ya wilaya ya misenyi wataendelea kupoteza
nyaraka zao mbalimbali zikiwemo za madai ya malipo na zile za kupandishwa madaraja.
Kwa
mujibu wa taarifa lilyorushwa na ITV ni kwamba baada ya uchaguzi wa
viongozi wa chama cha walimu wilaya ya misenyi,wamesema kuwa katika
kikao cha utekelezaji CWT imeutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya
misenyi kutatua migogoro ya waimu katika kipindi cha wiki mbili na
watakapokaidi chama cha walimu kitaitishwa mgomo kwa walimu wote wa
shule za msingi na sekondari bila kujali kuwa wakati huu ni wakati wa
kuandaa wanafunzi kufanya mitihani ya taifa.
Akijibu
malalamiko hayo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi
Bw. Moses Gwaza amekanusha vikali tuhuma hizo na kusema kuwa katika
kipindi cha miezi mitatu serikali imelipa madeni ya walimu katika wilaya
ya Misenyi zaidi ya shilingi miioni 338 na kwamba walimu 96 madai yao
hayapo kwenye bajeti ya mwaka huu na kuwataka kuwa na subira wakati
serikali ikijipanga kuwalipa.
0 comments:
Post a Comment