Friday 20 March 2015

Ugumu wa maisha ndio kipimo cha akili..!!!!!

Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu,lakini wakati mwingine ubunifu mwingine unaweza kukuweka pabaya.
Mmiliki wa Bar ya Siaya nchini Kenya,alimshtukia jinsia ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba jinsia yake sio ya kike,akatoa taarifa Polisi kuhusu mhudumu huyo, walipokuja kumpekua jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili.
Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar hiyo akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu wengine wa kike.
Polisi walimlazimisha avue nguo zake ili wamkague, wakaona hakuwa na muonekano wa jinsia ya kike, wanaendelea na upelelezi ili kujua ukweli japo Mkuu wa Polisi Kaunti ya Bondo amesema hata mmiliki wa Bar hiyo huenda akawa na makosa ya kumuajiri jamaa huyo bila kumkagua.

0 comments:

Post a Comment