Kompyuta nyingi zinaponunuliwa huwa na kasi kubwa, lakini baada ya muda kasi hiyo huanza kupungua.Kuna njia mbalimbali za kuongeza kasi ya kompyuta yako na vifaa vingine kama simu za mikono na Ipad.
Njia hizi zinaweza kutumika endapo kifaa chako
hakina shida kama vile uwezo wa kuhifadhi wa kifaa kuwa mdogo kuliko
programu unazotumia au kama kuna shida nyingine ya vifaa vilivyochomekwa
au vinavyotumika pamoja na kompyuta yako.
Kabla ya yote hakikisha kompyuta yako ina programu
ya kuilinda kama vile Antivirus au Internet Security. Watu wengi
wanapenda kuhifadhi vitu zaidi ya mara moja kwenye kompyuta. Hii
inachangia kuongeza vitu kwenye kompyuta na kupunguza nafasi kwenye
kifaa chako.
Njia bora ya kukabiliana na hali hii ni kutafuta
faili au folda e kwa kutumia ‘search’ au unaweza kutafuta programu ya
‘file dublicate’Hii itakuwezesha kutafuta nyaraka zote ambazo ziko zaidi
ya mara moja na kuziondoa na kisha kubakisha nakala moja tu.
Kwa faili za picha unaweza kutumia ‘Duplicate
Photo Cleaner’, hii itatafuta picha zote zilizohifadhiwa zaidi ya mara
moja, pia kuzifuta kwa minajili ya kuongeza nafasi kwenye kifaa chako.
Wakati unaingiza programu kwenye kompyuta au unapotembelea tovuti
mbalimbali, kuna faili zinazobaki kwenye kompyuta, hizi zinajulikana kwa
jina la ‘temporaly files’
Mafaili haya yanatakiwa kujiondoa yenyewe lakini haitokei mara kwa mara, matokeo yake yanabaki kwenye kompyuta na kuijaza.
Kwa hivyo unaweza kutumia programu ya Disk Clean
up ambayo iko kwenye kompyuta yako au unaweza kutafuta CCleaner na
Windows Advaced Care. Hizi ni programu zinazoweza kumaliza tatizo hilo
na mengine yanayofanana na hiyo .
Baadhi ya watumiaji wa kompyuta wanapenda kutumia
njia za mkato za kufungua programu (shortcuts) ili iwe rahisi kufungua
programu fulani, folda au vitu vingine kwa haraka. Ikumbukwe kuwa
shortcut zinapokuwa nyingi zinaweza kuharibu ‘desktop’ na kuleta
matatizo kwenye kifaa chako. Unashauriwa kuzipunguza au kutotumia kabisa
.
Kwa watumiaji wa Windows, waangalie vizuri.
Ukibonyeza upande wa kulia wa ‘mouse’ yako nenda sehemu ya shortcut
cleaner hii itaweza kukusaidia kumaliza tatizo .
Kuna kitu kinaitwa ‘Defragmentation’, maana yake
ni upangaji mzuri wa faili zako zilizopo ndani ya kompyuta. Hii
inafanyika kwa sababu unapotumia kifaa hiki kwa muda mrefu faili
zinaparaganyika halafu inachangia kufanya kifaa chako kwenda mwendo
mdogo. Hata hivyo, ukifanya defragmentation faili zako zitajipanga upya,
kwahiyo utatumia muda mfupi kutafuta kitu au kufungua kitu kwenye kifaa
chako.
Programu ya kufanya defragmentation iko kwenye
kompyuta yako moja kwa moja lakini kama unataka nyingine unaweza
kuangalia kwenye Advanced Windows Care niliyoitaja hapo juu itaweza
kufanya kazi hiyo.Ukiweka programu nyingi kwenye kompyuta yako,
utagundua kwamba kifaa chako kimeanza kwenda mwendo mdogo hasa wakati wa
kuwaka. Hatua hii inaitwa BOOT yaani hatua ya kompyuta kuwaka.
Kama mtumiaji wa kifaa unaweza kuamua unataka
programu zipi ziwake wakati kompyuta yako inawaka. Hapa unaweza kutumia
programu inayoitwa SOLUTO ambayo inapatikana bure kwenye mtandao .
0 comments:
Post a Comment