Friday, 27 March 2015

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India..!!!

Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.
Kulingana na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly Shivani Cherukuri kutoka Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh
aliweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kusajili alama 200 katika mashindano yaliyoandaliwa jumanne iliyopita.
Kulingana na jarida la Press Trust la India ,mtoto huyo alifuma mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na kisha umbali wa mita 7 na kujizolea alama 388.
Tukio hilo lilishuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
Dolly ambaye alizaliwa baada ya kupandikizwa kwa mbegu ya babake kufuatia kifo cha kakake katika ajali ya barabarani.
Kakake alikuwa mrushaji mishale wa kimataifa Cherukuri Lenin.
Babake Cherukuri Satyanarayana ,anasema kuwa Dolly alifunzwa kufuma mishale, tangu alipozaliwa.
Babake ni mmiliki wa klabu kimoja kinachofunza kurusha mishale.
Aidha aliiambia shrika la habari la AFP kuwa kitambo alikuwa amemptengezea uta na mishale nyepesi ilikukuza talanta ya mtoto huyo.
Sasa babake anasema kuwa anapanga kumshirikisha mwanawe katika mashindano kwa nia ya kumsajili katika vitabu vya rekodi za dunia za Guinness.


Related Posts:

  • WANAWAKE WAPIGWA MARUFUKU KUSAFIRI PEKE YAO LIBYA… Maafisa wa kijeshi wanaodhibiti eneo la mashariki mwa Libya, wametangaza marufuku kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 60 ya kuwazuia kusafiri nje ya nchi wakiwa peke yao. Marufuku hiyo inatajwa kutokana na sababu … Read More
  • NASA WATATANGAZA NINI KUHUSU MFUMO WA JUA? Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) leo linatarajiwa kutangaza ugunduzi "mkubwa" kuhusu mambo yaliyomo "nje ya mfumo wetu wa jua". Hafla ya kutangaza ugunduzi huo itapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya Nasa… Read More
  • KASHMIR:MARUFUKU MATUMIZI YA ANASA….. Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa. Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa. Idadi ya aina … Read More
  • JALADA LA MASOGANGE LAKWAMA KWA AG. Msanii  maarufu anayepamba  video za wasanii wa muziki wa bongo Fleva (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange ameendelea kusota rumande, huku jalada lake likiendelea kuwa mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Se… Read More
  • WABUNGE WAIDHINISHA KILIMO CHA BANGI UHOLANZI. Bunge la chini nchini Uholanzi, limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi. Mswada huo ulioidhinishwa utawakinga wakulima wa bangi, ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa. Mswada huo bado haujaidhini… Read More

0 comments:

Post a Comment