Mtoto aitwaye Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mama mzazi wa mtoto huyo Mwajuma Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo jijini Dar, amesema aliishi na mwanaye peke yake bila baba yake kwani walitengana Juni mwaka jana baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa muda mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa akimpeleka mwanaye nyumbani kwa wazazi wa mumewe kuwasalimia. Amesema baada ya kumkuta katika hali hiyo, alianza kuhangaika naye hospitalini kutafuta msaada, alipofika Temeke aliambiwa na madaktari kwamba kijana wake alikatwa vibaya na hivyo analazimika kufanyiwa upasuaji ili kumnusuru. Babu wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kufunguliwa shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani kwa madai ya ukatili.
IBKI ENTERPRISES YAZINDUA DUKA LA KISASA LA BIDHAA ZA HAIER UBUNGO
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KAMPUNI ya Usambazaji na Uuzaji wa Bidhaa za Haier, IBKI Enterprises Ltd,
imezindua duka la kisasa la uuzaji wa bidhaa za k...
3 hours ago







0 comments:
Post a Comment