Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha Picha na video chafu. Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema ''Marufuku kuchapisha picha au video chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa bila ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na picha hizo'' Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa makosa ya jinai uingereza na Wales. Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji watakaobainika kukiuka masharti mapya ''Anuani zao zitafungiwa'' Watumiaji wanaopeleka malalamishi Twitter kuhusu picha na Video zilizochapishwa watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia Kampuni kuwa hawakuwahi kutoa idhini ili kuchapisha picha au video mtandaoni na kuonekana kwa hadhira.
MHE. NDERIANANGA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS IFAD
-
NA. MWANDISHI WETU BERLIN, UJERUMANI
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na
Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekut...
23 hours ago
0 comments:
Post a Comment