Monday, 16 March 2015

Mwanamke mwenye 'sura mbaya' atoa filamu..

Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.
Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani.
Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye.
Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie.

Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''.
Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi.
Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo.
Mwanamke huyo pia anafanya kazi na Tina Meir ambaye mwana wao Mega alijiuwa baada ya kuonewa katika mtandao.

Related Posts:

  • Serikali ya muungano ya Palestina kujiuzulu...!!! Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahammud Abbas ametangaza kuwa serikali ya muungano aliyounda na Hamas mwaka jana itajiuzulu. Abbas hakutangaza ni lini hasa hatua hiyo itachukuliwa lakini inatarajiwa hatua hiyo itate… Read More
  • Shambulio lafanyika Kanisa la Marekani…!! Shambulio katika Kanisa la Kihistoria la Methodist katika jimbo la South Carolina, MarekaniPolisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani, wanamsaka mtu mwenye silaha alihusika katika shambulio katika Kanisa la Metho… Read More
  • Sura ya mwanamke kuwa katika noti mpya…… Benki Kuu ya Marekani Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja, noti mpya ya dola kumi nchini Marekani itakuwa na picha na mwanamke. Wizara ya Fedha ya Marekani imewataka wananchi wa Marekani,kutoa mawaz… Read More
  • Ramadhani imeanza leo maeneo mengi ya dunia!! Waislamu katika nchi nyingi duniani leo wamenza funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Taasisi husika katika nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu zilitangaza jana jioni kwamba, Alkhamisi ya leo tarehe 18 Juni i… Read More
  • Je unakifahamu kiungo cha Giligilani? Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheni habari kemkem kuhusu afya.                        … Read More

0 comments:

Post a Comment