Friday, 6 March 2015

Ronaldo huijali mno Sanamu yake

Cristiano Ronaldo mara zote amekuwa na maamuzi ya kipekee yasiyo pitia kwa mtu wa pili na likija suala la kujijali ama kujipenda humwambii kitu hutekeleza ,suala ambalo limemfanya aonekane mchezaji wa kipekee mkubwa na imemjengea heshma kubwa. Lakini mkali huyu wa kabumbu anayesukuma gozi Real Madrid katika kujipenda amepiga hatua moja mbele yenye kuzua mjadala katika mitandao ya jamii na miongoni mwa watu wanaomfahamu ,na kama kinachosema na mtunza makumbusho wa timu Real Madrid ambaye kazi yake kubwa ni utunzaji wa sanamu za wachezaji na kuhakikisha hazipauki na kubaki kama wachezaji halisi walivyo . Gonzalo Presa, ndiye mhifadhi mkuu wa makumbusho hayo ya timu wa Real na ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Museo de Cera ,ametema kwamba Ronaldo hutuma kinyozi wake binafsi mara moja kwa mwezi kuhakiki sanamu inayofanana naye iwe na muonekano anaoutaka. Na anasema kwamba Cristiano huwa anataka sanamu hiyo ichanwe nywele mara moja kwa mwezi,na nywele za sanamu hiyo zimeagizwa kutoka nchini India ni nywele halisi . Ronaldo mwenyewe ana makumbusho yake binafsi nchini Ureno,na makumbusho hayo yameendelea kuonesha mambo yamhusuyo tangu mwezi December,mwaka 2013.

Related Posts:

  • DARAJA LAPOROMOKA NA KUWAUA 10 INDIA… Takriban watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya daraja moja la juu lililokuwa likijengwa kuporomoka, kwenye mji wa mashariki mwa India wa Kolkata Ripoti zingine zinasema kuwa karibu watu 150 huenda wa… Read More
  • RIPOTI: DUNIA YAELEMEWA NA WATU WANENE..! Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani. Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo … Read More
  • AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA KUMUUA RAIS MAGUFULI…. Kondakta Hamimu Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka kumtishia kumuua kwa maneno Rais Dk. John Magufuli kwa kujitoa mhanga. Wakil… Read More
  • SERIKALI KUNUNUA NDEGE MBILI, MELI…. Serikali imepanga kununua ndege mbili mpya na meli moja kwa ajili ya Ziwa Victoria katika siku chache zijazo, imefahamika. Mpango wa kununua ndege ulitangazwa jana na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipozung… Read More
  • KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA JINGINE BAHARINI… Wanajeshi wa Korea Kusini wanasema kuwa, Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu katika eneo la pwani ya mashariki ndani ya bahari, wakati ambapo rais Barrack Obama anaongoza kikao cha dunia kuhusu usalama wa … Read More

0 comments:

Post a Comment